BUSINESS AND SOCIAL ENTREPRENEURS BLOG...ASSISTANCE TO ENTREPRENEURS AND START UP FOUNDERS IN FINDING BUSINESS IDEAS, FUNDING, ADDRESSING PROFESSIONAL ISSUES,EXECUTIVE MENTORING AND BUSINESS NETWORKING..CONTACT US FOR MORE INFORMATION, EMAIL: innombele2001@yahoo.com, PHONE: +255(0) 765 571 301

Sunday, September 3, 2017

CALIHE: ASALI BORA NA MAAJABU YAKE KATIKA AFYA YA MWANADAMUWadau wa bidhaa ya Calihe wakifurahia bidhaa hizo.


CALIHE HONEY ni jina la asali yenye mchanganyiko wa vitu vinne, yaani Mlonge(majani yake), mdalasini india, karafuu na tangawizi. Lengo la muunganiko huo ni kuifanya iboreke zaidi na kuwa lishe au tiba kwa mtumiaji.

Lishe maana yake inatumika kwa mtu yeyote bila kujali rika mf. Mtoto, mjamzito, mtu mzima, anae au hata asiye umwa. Lishe hii inaweza kutumika kama huduma ya kwanza nyumbani kwako kwani inaweza kukusidia kutibu magonjwa mengi mno, mfano tumbo la kuuma, vidonda tumbo, kifua cha kubana, kikohozi na hata pumu. Sifa yake kubwa mwilini ni kupambana na lehemu(cholestrol), kinga ya mwili, mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kuondoa sumu sumu zote mwilini, kuzibua na kuipa nguvu mishipa ya kizazi pamoja na mishipa mingine n.k. inaanza kufanya kazi kuanzia hapohapo unapoitumia na kutoa matokeo ya nafuu au kupona kabisa magonjwa mbalimbali mwilini kuanzia au ndani ya siku sita...

Kwa order ya jumla na rejareja wasiliana na :-

Mr. Calvin Salema-0745 896 886

Wednesday, April 19, 2017

DONDOO KUHUSU SOKO LA HISA NA MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA HISA


SEHEMU YA PILI:

1.       UTANGULIZI:
Katika sehemu ya somo iliopita tumeangalia mambo kadha wa kadha, ikiwemo, nini maana ya soko la hisa, nini maana ya Hisa, Tumeangazia faida za kuwa soko la hisa, tumeangazia faida za kuwekeza katika hisa na Hatimaye changamoto zitokanazo na uwekezaji katika soko la hisa. Naamini somo hili limekua la barka sana kwako na limekupa mwangaza angalau wapi kwa kuanzia.Katika somo la leo tutaangalia kwa undani mambo ya kuzinagatia kabla ya kufanya uwekezaji huu; tutaangalia vigezo utakavyotumia kuipima kampuni ama sekta na kujua endapo ni sehemu nzuri kwako kuwekeza kwa kununua hisa zake. Nipende kuchukua fursa hii kuwa karibisha wote katika darasa letu la Hisa. Karibuni Johnbosco Mvile2.       MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA HISA ZA KAMPUNI HUSIKAKama tulivyokwisha ona awali ununuzi na uuzaji hisa unachangamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuathiri kiwango cha faida unachoweza kukipata kutoka na kuuza hisa hizo. Lakini hili linaweza kuzuiwa endapo mnunuzi atazingatia vigezo muhimu katika kuchagua Kampuni yenye viashiria chanya vya bei ya hisa zake kuleta faida mbeleni. Hili ni kutokana na ukweli kwamba kama mwekezaji sehemu kubwa ya faida utaweza kuipata endapo utaamua kuziuza hizo hisa baadae kwa matarajio ya kupata faida.  Jambo la msingi sana ambalo ni muhimu kuwa nalo katika mipango yako si tu kununua hisa ili uwe sehemu ya mmiliki wa Kampuni husika bali kua mfanyabiashara ya kuuza na kununua Hisa. Kwa sababu ni rahisi kuishia kununua hisa za kampuni husika na kuishia kua na Hisa na kungoja Gawio ambalo huna uhakika endapo litatolewa ama la na kiasi gani hujui. Hivyo msisitizo ni muhimu uwe katika kuuza na kununua hisa kwa siku za baadae.Mpaka sasa katika soko la Hisa la Dar es salaam kuna jumla ya makampuni 25, ambayo yanauza hisa, kwa hiyo uwanja ni mpana; sio lazima uangalie kampuni mmoja tu, jaribu kufanya utafiti hata kwa kampuni ambazo zipo tayari katika soko la hisa kuona endapo unaweza kuwekeza na kupata faida.Kupitia kujenga fikra za kiuwekezaji namna hii na tuangalie vigezo kadha wa kadha ambavyo vitakupa kiashiria kuwa unapowekeza pana uwezekano wa kuwa na usalama na kiwango kidogo cha kupoteza kutokana na mabadiliko ya soko kiujumla.

Lakini pia hii itakusaidia hata ikiwa na kampuni yako na ukawa na hitaji kukuza mtaji kwa njia ya hisa –ni vigezo gani vitafanya hisa za kampuni yako kuuzika kwa urahisi na hivyo kuwe kupata mtaji wa kutosha kuweza kuimarisha biashara yako; kwa sababu huu ndio mfumo ambao makampuni makubwa yote ulimwengu yanaongozwa na kuendeshwa. Mfano. Facebook, Microsoft etc

KIGEZO#1: ANGALIA ASILIMIA YA UMILIKI WA SOKO YA KAMPUNI HUSIKA(Market share)

Kikawaida kampuni yenye asilimia kubwa ya soko, inakuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza faida na hivyo kuendelea kupanda kwa bei za hisa zake kwa siku zijazo kutokana na wawekezaji wengi kuvutiwa na kampuni zinazo pata faida. Taarifa hizi unaweza kuzipata katika kitabu cha taarifa (Prospectus) ya kampuni husika. (Tembelea link Katika sehemu ya 4 ya somo kujua Taarifa za Vodacom)KIGEZO#2: ANGALIA SERA YA GAWIO YA KAMPUNI(Dividend Policy)

Kila kampuni ina sera yake ya namna ya ugawaji gawio. Sera hiyo huweza kueleza masharti na vigezo katika ugawaji gawio mathalani kiwango cha asilimia na kipindi cha muda ambacho kampuni inatarajia kutangaza gawio  kwa wanahisa wake. Kujua hili kutakusaidia kufanya maamuzi ya kununua hisa za kampuni husika ama kutonununua kutokana na mipango ama matarajio yako juu ya uwekezaji wa hisa.KIGEZO#3: ANGALIA KASI YA UKUAJI WA KAMPUNI (Growth rate)

Mara nyingi ukuaji wa kampuni huenenda na ongezeko la bei ya hisa zake. Hii ni kutokana na kukua kwa jumla kwa thamani ya kampuni husika kunakotokana na kasi ya ukuaji wake unaozingatia ongezeko la mtaji, na mali za kampuni husika kwa ujumla. Ukuaji wa Kampuni unapimwa kwa kuangalia jumla ya mali zote za kampuni ukilingalinisha na vipindi vilivyopita; Lakini pia kiasi cha Mauzo na Faida kinachopatika ukilinganisha na vipindi vilivyopita. Taarifa hizi pia utazipata katika kitabu cha taarifa cha Kampuni. (Tembelea link Katika sehemu ya 4 ya somo kujua Taarifa za Vodacom)KIGEZO#4: ANGALIA AINA YA MWEKEZAJI MAMA WA KAMPUNI(Strategic Investors)

Kila kampuni ina mwekezaji mama, ama mwanzilishi wa kampuni. Ni muhimu kuzingatia hili kwani mara nyingi mwekezaji mama ndio huwa anamiliki sehemu kubwa ya hisa na hivyo kuwa na sauti katika maamuzi mengi yanayofanywa kuhusu kampuni husika. Lakini Pia mwekezaji mama anajukumu la kusimamia uongozi wa kampuni kuhakikisha nidhamu, na mali za kampuni zinalindwa, rushwa na ubadhirifu wa mali za kampuni hautokei. Hivyo ni muhimu kujua nani ni mwekezaji mama kwani kesho ya kampuni husika inategemea sana mwekezaji mama. Mwekezaji mama mzuri ni lazima awe na Fedha za kutosha, Utaalam/Ujuzi wa sekta iliomo kampuni, pamoja na uwezo wa kutosha kusimamia kampuni.KIGEZO#5: ANGALIA UKUAJI WA MAUZO YA KAMPUNI KWA KILA MWAKA ( Revenue Growth)

Mauzo ndio uhai wa kampuni, endapo mauzo yanapungua icho ni kiashiria kibaya kwa uhai wa kampuni husika. Hivyo kuna weza kuathiri bei ya Hisa kwa siku zijazo. Hivyo ni muhimu kuwekeza katika kampuni ambayo Mauzo yake yanaongeza ama kukua kwa asilimia isiyo chini ya asilimia katika sekta husika.KIGEZO#6: ANGALIA BIDHAA INAYOUZWA,UHITAJI WAKE SOKONI (Product Demand)

Baadhi ya bidhaa zinazouzwa na makampuni zina athiriwa sana na nguvu ya mabadiliko ya teknolojia. Mfano sekta ya mawasiliano. Hii inaweza kufanya bidhaa inayouzwa leo ikawa haihitajiki  baada ya kipi fulani cha muda. Hii inaweza kuathiri sana ukuaji wa Kampuni na uwezo wake wa kutengeneza faida na hivyo kuathiri bei ya hisa zake pia. Mfano Makapuni ya simu kwa sasa yanategemea sana mapato yake kutoka kwenye mauzo ya huduma ya mtandao(Data). Kuliko kutoka katika simu zinazopigwa. Mfano pia Kampuni kadhaa za mawasiliano zilikufa kutokana na uwezo wake mdogo wa kuendana na teknolojia mfano. Nokia, Errkson, Black Berry n.kKIGEZO#7:ANGALIA UWIANO WA MADENI NA MTAJI WA KAMPUNI(Debt to Equity Ratio)

Endapo kampuni ina madeni kuzidi mtaji wake. Hii inaashiria kuwa kuna uwezekano mdogo wa kampuni hiyo kulipa gawio kwa siku zijazo kutokana na sehemu ya faida kutumika katika kulipa madeni.KIGEZO#8: ANGALIA KIWANGO CHA FEDHA KINACHOWEKEZWA KATIKA MAENDELEO KAMPUNI(Capital Expenditure)

Hii inamaana kuwa kama kampuni inautaratibu wa kutumia sehemu ya faida yake katika fedha za maendeleo yaani kujiimarisha inakuhakikishia kama mwekezaji kuwa thamani ya kampuni itaendelea kupanda siku hadi siku. Na kama tulivyo ona mara nyingi thamani ya kampuni huendana na thamani ya bei ya hisa. Lakini pia ni kiashirio kuwa kampuni ina mikakati kwa siku zijazo ya kuendelea kufanya vizuri katika soko na uzalishaji kwa ujumla.KIGEZO#9:ANGALIA UWEZO WA KAMPUNI KUTENGENEZA FAIDA  (Profit )

Kampuni yenye kutengeza faida inakuhakikishia kuwa kutakua na gawio lakini pia ina wavutia wawekezaji wengi na hivyo bei ya hisa zake kuwa juu.KIGEZO#10: ANGALIA SERA ZINAZOWEZA KUATHIRI MWENENDO WA UKUAJI WA SEKTA ILIMO KAMPUNI HUSIKA.

Hili ni gumu kidogo lakini kupitia mamlaka husika unaweza kutabiri aina ya mabadiliko ya kisera yanayoweza kutokea katika sekta husika siku zijazo na endapo yatakua na athari zipi katika soko la Hisa.

KIGEZO#11: ANGALIA UIMARA WA UONGOZI WA KAMPUNI HUSIKA(Management team)

Hii itakujengea ujasiri katika ufanisi wa kampuni husika. Uongozi wa kampuni mzuri ni ule unaoweka masahi ya wawekezaji mbele katika kutekeleza majuku na malengo ya Kampuni. Aina hii ya Uongozi wa kampuni huwavutia wawekezaji wengi kutokana na Kampuni nyingi zenye uongozi imara hufanya vizuri sokoni na hivyo kupelekea hisa zake kupata hata siku za baadae.

Kwa kuzingatia baadhi ya vigezo tulivyoshirikishana naamini utakua katika wakati mzuri wa kufanya maamuzi ya kununua wapi ama kwa nani na kuuza hisa zako wapi na lini.

3.       UTARATIBU WA KUNUNUA HISA NA KUUZA HISA

Baada ya kuyazingazia hayo tuliokwisha kujifunza ufuatao ni ufupisho wa namna ya kununua na kuuza hiza zako katika soko la hisa. Kwa maelezo zaidi fuatilia link za tovuti zao zifuatazo katika sehemu ya 4 ya somo:

i.                     Ununuzi

Mwekezaji anayetaka kununua hisa atafuata taratibu zifuatazo:

a)      Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kununua hisa

b)      Jaza fomu maalum za kununua hisa na kulipia hisa unazotaka kununua

c)       Dalali ataweka fedha kwenye akaunti maalum ya benki kwa ajili ya kununua na kuuza hisa za wateja

d)      Dalali ataweka oda yako ya kununua hisa akitumia namba maalum ya mteja.

e)      Iwapo bei unayotaka kununulia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kuuza, basi atakuwa amekununulia hisa hizo. Mwekezaji atapokea cheti cha kuthibitisha kuwa ni mwekezaji kwenye kampuni hiyo.ii.                   Uuzaji

Mwekezaji anayetaka kuuza hisa atafuata taratibu zifuatazo:

a)      Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kuuza hisa

b)      Kabidhi hati yako ya umiliki wa hisa kwa dalali

c)       Dalali atahakiki umiliki wa hisa hizo kabla ya kuuza. Kama hisa haziko kwenye hifadhi ya hisa, dalali ataziweka kwenye hifadhi kabla ya kuuza

d)      Dalali ataweka oda yako ya kuuza hisa akitumia namba maalum ya mteja. Iwapo bei unayotaka kuuzia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kununua, basi atakuwa amekuuzia hisa hizo na mwekezaji atalipwa4.       BAADHI YA VYANZO MUHIMU VYA TAARIFA VITAKAVYOKUSAIDIA.

ü  Namna ya kujiorodhesha kwenye soko la Hisa endapo unakampuni yako.
ü  Anwani za washauri walioidhinishwa wa maswala ya uwekezaji katika soko la Hisa
ü  Anwani za Wakala ukusanyaji(Brokers/Dealers) walioidhinishwa
ü  Taarifa za kifedha za kampuni ya Vodacom na namna ya ununuzi wa hisa zake           

                                                                   ----------------------------MWISHO-----------------------------------

Kwa ufafanuzi na maelezo Zaidi wasiliana na mwandishi kwa anwani ifuatayo: 
Name:Johnbosco Mvile
Email: mvilej@gmail.com
Mobile phone: 0714206230

Tuesday, April 18, 2017

DONDOO KUHUSU SOKO LA HISA NA MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA HISAMWANDISHI: Johnbosco Mvile; BA Acc, CPA(T)

SEHEMU YA KWANZA:

1.       UTANGULIZI

Ndugu msomaji Napenda kuwa karibisha Katika somo hili kuhusu “Dondoo kuhusu soko la Hisa Na mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kununua HISA”. Somo hili ni muhimu kwani ni somo linaloendana na wakati tuliopo. Kulingana na utaratibu uliopo makampuni ya simu karibu yote yatalazimika kuuza hisa zao Katika soko la hisa la Dar es Salaam. Hili limekuja ili kisaidia wananchi wazawa kupata sehemu ya umiliki wa makampuni hay na hatimaye kununufaika kutokana na kipato(faida) inayotengenezwa na makampuni haya. Katika semina hii tutaangalia vipengele vifuatavyo:SEHEMU YA KWANZA:

·       Maana ya soko la hisa

·       Umuhimu wa soko la Hisa

·       Maana ya Hisa

·       Faida ya kumiliki/kuwekeza katika Hisa

·       Changamoto za uwekezaji katika Hisa

            SEHEMU YA PILI

·       Mambo ya muhimu kuzingatia kabla ya kununua hisa za kampuni husika

·       Utaratibu wa Kununua HISA na  kuuza HISA

·       Baadhi ya vyanzo muhimu vya taarifa vitakavyokusaidia
2.       NINI MAANA YA SOKO LA HISA(DHAMANA)

Ni mahali ambapo hisa zinanunuliwa na kuuzwa. Wakati mwingine tunaweza kuliita ni soko la mitaji. Ni mahala ambapo taasisi zinaweza kujipatia mtaji kutokana na mauzo ya hisa zake, na kufanya umma kupata nafasi ya kumiliki sehemu ya mtaji wa kampuni hilo. Pia kuyawezesha makampuni hayo kukua na kupanua huduma ama shughuli zake ambazo zinaweza pelekea ongezeko la ajira na kipato kwa nchi na wananchi kwa ujumla.

Kwa Tanzania soko hili linaitwa solo la hisa/dhamana la Dar es salaam (Dar es salaam stock of exchange). Ni soko sawa masoko mengine ya bidhaa tofauti. Soko la hisa la Dar es salaam lilianzishwa mnamo mwaka 1996 na mpaka sasa lina umri upatao miaka 21 huku ikiwa na jumla ya Kampuni 25 zilizojiandikisha na kuuza hisa zao katika soko hili. Katika soko la Hisa utakutana na wadau wafuatao :

·       WAWEKEZAJI(MAKAMPUNI AMA WATU BINAFSI)
Ni makampuni ama watu binafsi wanao fanya biashara ya kuuza na kununua hisa na dhamana nyinginezo katika soko la Hisa. Mfano ; TOL Gases Ltd. (TOL), Tanzania Breweries Ltd. (TBL), CRDB Bank. (CRDB) n.k
·       WASHAURI UWEKEZAJI WALIOIDHINISHWA:
Hawa ni washauri rasmi wa masuala ya uwekezaji katika hisa na dhamana nyingine zinazouzwa katika soko. Unaweza kuwapata kupitia link nitazozorodhesha mwishoni mwa somo

·       WAKALA UKUSANYAJI (DEALERS/BROKERS) WALIOIDHINISHWA 
Madalali (brokers) : Hawa ni walioidhinishwa kufanya kazi kama wakala (agent) kwa niaba ya wanunuzi na wauzaji tu. Na hawaruhusiwi kununua hisa/dhamana kwa ajili yake.

Wachuuzi (dealer) :Hawa ni walio idhinishwa kununua hisa au dhamana nyinginezo kwa niaba yake mwenyewe (principal) na vile vile kwa ajili ya wateja kwa usimamizi wa  Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.

3.       UMUHIMU WA SOKO LA HISA

Soko la hisa lina mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi. Pia ni kiashiria kikubwa cha hali ya uchumi kwa ujumla. Mojawapo ya faida ya kuwa na soko hili ni.

·       Upatikanaji wa mitaji kwa Makampuni.

·       Kusaidia katika upatikanaji wa mitaji kwa makampuni

·       Kusaidia wananchi kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba

·       Kuongeza maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza

·       Ni kiashiria mojawapo cha ukuaji wa uchumi wa nchi

·       Kunaongeza dhana ya uwajibikaji na uendshaji mzuri kwa makampuni yaliyoorodheshwa

·       Kunasaidia pia katika kuwapa nafasi umma kuwa na umiliki katika makampuni yaliyo orodheshwa.


4.       NINI MAANA YA HISA

Hisa ni umiliki; unaponunua hisa maana yake unataka kuwa sehemu ya mmiliki wa kampuni inayouza hisa( kampuni inayouza umiliki wake). Mfano Vodacom wameamua kuuza 25% ya umiliki wa kampuni yao. Ikiwa na maana kuwa mara baada ya zoezi la uuzaji hisa kukamilika 25% ya thamani zima ya vodacom Tanzania itakua inamilikiwa na Watanzania hii ni sawa na Tsh 476bilioni. Na bei ya Kila hisa moja ni Tsh 850, na unatakikwa kununua kiwango cha chini cha Hisa 100. (Vodacom Tanzania(2017), IPO,Prospectus,pg 12)


5.       FAIDA ZA KUMILIKI/KUWEKEZA KATIKA HISA

·       Ni moja ya njia za kujiwekea akiba

Unapo nunua Hisa unaweka akiba, na mara unapoihitaji pesa hiyo unaweza kuipata kwa njia ya kuiuza hizo hisa ulizo zinunua.

·       Inakupa umiliki wa kampuni husika na hivyo kuwa na maamuzi kutegemea kiwango cha hisa unazomiliki.

·       Hisa zinaweza utumika kama dhamana kwa ajili ya kuombea mkopo benki

·       Endapo bei ya hisa itapanda ukilinganisha na bei ulionunulia unajihakikishia kupata faida kubwa endapo utaamua kuziuza.

·       Kupata gawio endapo kampuni itapata faida;

·       Uwekezaji kwa njia ya Hisa kunakufanya uokoe Muda. Pesa unayoiwekeza kwa njia ya ununuzi wa Hisa inaweza kukuletea faida bila wewe kuhusika moja kwa moja katika shughuli za kampuni hiyo uliowekeza.
CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI KATIKA HISA

Kwanza ijulikane kuwa soko la hisa linaendeshwa na Nguvu ya Uhitaji na Upatikanaji wa Hisa. (demand and Supply forces). Mabadiliko katika nguvu hizi ndio yanayo amua bei ya hisa sokoni iwe kiasi gani. Na hatimaye kiasi cha faida utakachopata kutokana na kuuza ama kununua hisa Hizo. Endapo uhitaji utazidi utazidi upatikanaji wake(suppy), marazote bei ya hisa hizo itakua juu. Na mara uhitaji wake unaposhuka bei ya hisa pia hushuka.

Mara zote katika uwekezaji katika soko la Hisa, mwekezaji anatarajia kupata faida kubwa kutokana na uuzaji wa Hisa zake zaidi kuliko faida itokanayo na gawiwo inalopatika mwishoni mwa mwaka endapo kampuni itakua imepata faida. Lakini ijulikane kuwa haki ya Gawio si ya moja kwa moja. Hakuna hakikisho (guarantee) kuwa lazima gawio litalipwa hii itategemea  mwendeno mzima wa kampuni pamoja na maamuzi ya wakurugenzi wa kampuni baada ya kuzingatia mahitaji ya kuwekeza ndani ya kampuni yenyewe kwanza katika kuiimarisha kabla ya kupendekeza kiasi cha gawio litakalolipwa kwa wawekezaji.

Hivyo basi uwekezaji katika soko la hisa huweza kuathiriwa na mambo mbalimbali ambayo yanaweza kufanya mwekezaji ashindwe kupata kiasi cha faida alichotarajia endapo ataamua kuziuza hisa hizo kutokana na kushuka kwa bei ya kuuzia ukilinganisha na bei alio nunulia awali. Baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo.

·       Mabadiliko katika mwenendo wa uchumi wa Nchi

·       Hali ya kifedha ya Kampuni husika

·       Mabadiliko sera katika sekta husika uliyowekeza

·       Mabadiliko ya kiutawala katika kampuni husika

·       Kuongezeka kwa ushindani wa kibiashara katika sekta husika

Hivyo changamoto kubwa inakaa katika uwezo wa mwekezaji kuweza kutabiri vizuri endapo bei ya hisa za kampuni husika itapanda mbeleni endapo mwekezaji ataamua kuziuza. Swali ambalo ni changamoto hapa ni kujua endapo bei ambayo Kampuni imeamua kuuza hisa zake ni minimum ikiwa na uwezekano wa kuongezeka baadae ama ni maximam ikiwa haina uwezekano wa kuongezeka siku zijazo.

Lakini pia jambo jingine ambalo ni gumu tabiri ni endapo watu wengi watanunua hisa za kampuni husika, je ni mbeleni kutakuaje. Kuna mambo mawili hapa

-          Mbeleni watu wengi watakua na hisa za kampuni husika, na matokeo yake hapatakua na wa kumuuzia mwenzake hivyo bei kushuka, na hatimaye kuuza kwa hasara.

-          Mbeleni watu wataaendelea kununua hisa za kampuni husika, labda kutokana na hali nzuri ya kifedha na ukuaji mzuri wa kampuni husika na hivyo basi kuendelea kuwavutia wengi. Hili litaafanya bei ya Hisa kuuendelea kuwa juu na kwa mwekezaji atakaye amua kuziuza atapata faida.

Kwa ufafanuzi na maelezo Zaidi wasiliana na mwandishi kwa anwani ifuatayo: 
Name:Johnbosco Mvile
Email: mvilej@gmail.com
Mobile phone: 0714206230


Monday, April 3, 2017

VITABU MUHIMU VYA AWALI KATIKA UTUNZAJI KUMBUKUMBU WA BIASHARA YAKO

1. Kitabu cha Stakabadhi (Receipt Book)Utunzaji wa kumbukumbu za Biashara ni muhimu sana katika kuhakikisha uthibiti mahususi wa mwenendo wa mapato na matumizi katika biashara. Tafiti zinaonesha kutotunza kumbukumbu za biashara vizuri, ni mojawapo ya sababu ya biashara nyingi kufa.

Katika  utafiti mdogo niliofanya, changamoto ya utunzaji kumbukumbu inawakabili sana wafanya biashara wadogo na wakati.

Hivyo basi makala hii fupi na zijazo zitaangazia katika namna ya kutatua changamoto hii inayowakabili wafanya biashara wengi.

Tuanze kwa kuangazia vitabu muhimu vya awali vinavyohitaji mara unapoanza biashara yako kama ifuatavyo:(minimum required bookkeeping books)


2. Kitabu cha hati ya Madai(Invoice Book)
3. Kitabu cha hati za Malipo (Payment Voucher)


1. KITABU CHA STAKABADHI (Receipt Book)
Hiki ni kitabu kwa ajili ya kupokelea fedha taslimu. Kitabu hiki kinatumika kutunzia kumbukumbu zinazoonesha kiasi cha fedha zilizopokelewa na kutoka wapi. Kwa kawaida kitabu hiki huwa na kopi mbili moja inabaki kwenye kitabu na ya pili unampa yule ambaye umepokea fedha Taslimu kutoka kwake.

Mfano wa Stakabadhi/Receipt
2.KITABU CHA HATI YA MADAI
Hiki ni kitabu kinachotumika kutunzia hati za madai endapo umetoa huduma ama kuuza bidhaa kwa mkopo. Kitabu hiki pia kina kopi mbili moja unampa mdaiwa, na moja unabaki nayo kwenye kitabu kama kumbukumbu yako.


Mfano wa Hati ya Madai/Invoice

3. KITABU CHA HATI ZA MALIPO(Payment Voucher)
Hiki ni kitabu kinacho tumika kutunza hati za malipo yanayofanyika katika biashara yako. Mfano endapo unahitaji pesa kwa ajili ya kulipia bili ya umeme; inatakiwa uandike hati ya malipo kuidhinisha malipo hayo ya umeme, inashauriwa hati hii isainiwe mara zote na mtu zaidi ya mmoja, kama njia mojawapo katika udhibiti wa fedha za biashara yako.


Mfano wa Hati ya Malipo.


Tutaendelea kuangazia masuala mbalimbali muhimu katika utunzaji wa kumbukumbu za bishara yako ikiwa ni pamoja na uthibiti wa fedha katika biashara yako.

Ukiwa na maswali ama uhitaji wa ushauri juu ya utunzaji kumbukumbu za biashara yako na mambo mengine ya kitaalamu yahusiyo biashara wasiliana nasi.Mr. Johnbosco Mvile

Simu: +255 763895490

Email: mvilej@gmail.com


VIDOKEZO MUHIMU UNAPOANDAA MPANGO WA BIASHARA YAKO (BUSINESS PLAN)


Kuandaa mpango biashara(Business Plan) ni muhimu sana kabla ya kuanza kufanya biashara yoyote. Si tu kwa sababu unahitaji pesa toka Taasisi za kifedha bali kuweza kuielewa biashara yako, na kujiapanga kisaikolojia na kifedha.


Unapoandaa Mpango wa biashara yako ni muhimu kuzingatia ipengele vifuatavyo.

1. Aina na Soko la bidhaa yako(Market analysis)
2. Namna ya uendeshaji          (Business Management)
3. Vyanzo vya Mtaji                  (Capital budget)
4.Ushindani uliopo                    (Competition)
5. Makisio ya Hali ya kifedha    (Financial Projection)


1. AINA NA SOKO LA BIDHAA YAKO
Katika kipengele hichi jiulize maswali yafuatayo:

      a)Ni aina gani ya bidhaa au huduma utakazo uza?(taja sifa na Faida ya hiyo bidhaa)
      b)Ni kwanini watu wanunue kwako na si kwa mwingine?

2. NAMNA YA UENDESHAJI BIASHARA
Katika kipengele hiki jiulize maswali yafuatayo:

     a) Je wewe na watu utakaoshirikiana nao katika bishara, mna ujuzi na utaalamu unaotakiwa?
     b) Idadi yenu inatosha?
     c) Nini sera na sheria zinazotawala na kuongoza aina ya biashara mnayoendesha?

3. VYANZO VYA MTAJI/FEDHA
Katika kipengele hiki jiulize mambo yafuatayo:
   
     a) Je mtaji nilionao unatosha kuanza biashara?
     b) Je Vyanzo vipi vingine mbadala endapo mtaji hutatosheleza?

4. USHINDANI ULIOPO SOKONI
Katika kipengele hiki ni muhimu kujiridhisha kwa kujiuliza mambo yafuatayo:

     a) Nani ni mshindani wako mkubwa
     b) Ni mambo gani unaweza kujifunza kutoka kwake
     c) Umejipanga vipi kukabiliana na ushindani huo (unajitofautishanaje?)

5. MAKISIO YA HALI YA KIFEDHA
 Katika kipengele hiki ni muhimu kuzingatia yafuatayo; Ikiwa huna uzoefu na mambo ya fedha ni vizuri kumwona mtaalamu ili kutofanya makisio yalio mbali na uhalisia.

     a)Wastani wa Mauzo utakayopata (kwa mwaka ama kwa mwezi)
     b)Wastani wa gharama za kununua bidhaa (kwa mwaka ama mwezi)
     b) Gharama za uendeshaji biashara(kwa mwaka ama kwa mwei)
     c) Faida utakayopata ukichukua Jumla ya mauzo kutoa Gharama za Manunuzi Bidhaa na Gharama za uendeshaji)

Pia kutokana na makisio hayo unatakiwa uwe na uwezo wa kujua yafuatayo:

     a)Kiasi gani cha mauzo kinatakiwa kwa siku/kwa mwezi ili kuweza kufidia gharama    
         zote za uendeshaji pasipo kupata faida.
     
b) Ni gharama zipi ninapanda/kubadilika kulingana na uzalishaji/kukua wa biashara
        yako na zipi ambazo ni hazibadiliki kulingana na kukua kwa biashara yako.


Kwa ufafanuzi wa kina juu ya kuandaa mpango wa biashara yako wasiliana na mwandishi, Usikose kuendelea kufuatilia mkala zetu. 

Johnbosco Mvile
+255763895490
mvilej@gmail.com


MBINU ZA UDHIBITI WA GHARAMA ZA UENDESHAJI BIASHARA/TAASISI

Katika kipindi ambacho biashara nyingi zinafungwa, huku gharama za uendeshaji zikizidi kupanda kutokana na mabadilikomakubwa ya kiuchumi ambayo yameathiri mzunguko na upatikanaji wa pesa.  Kujua mbinu za uthibiti wa gharama za kiuendeshaji ni jambo lisiloepukika.

Wamiliki wa biashara/taasisi waliona uelewa wa kutosha juu ya uthibiti wa gharama za kuendesha biashara ndio wanaoweza kukwepa adha ya kufunga biashara zao ama kuuza biashara zao.

Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea biashara kufungwa ama kufirisika mara hali ya mazingira ya kibiashara na uchumi yanapobadilika, miongoni wa sababu hizo ni.

·          Kutokuwa na mipango mikakati ya kuthibiti gharama za kiuendashaji biashara

·          Kuwa na mfumo dhaifu wa kiuendeshaji biashara-unaotegemea vyanzo visivyo vya kudumu na visivyo vya uhakika katika uanzishaji na uendeshaji biashara.

·          Kutohimiza mazingira ya ndani ya kibunifu yanayozingatia hali ijayo ya kibiashara na kiuchumi na hivyo kupelekea kujipanga mapema.

·          Kuwa na mfumo dhaifu wa upatikanaji na usambazaji wa taarifa sahihi zinazohusu uendeshaji biashara na hali ya biashara kiujumla. Hii ni pamoja na kutokua na utunzaji kumbukumbu mzuri kutokua na wataalam.

·          Kuwa na uthibiti wa fedha dhaifu. Hii ni pamoja na kutokua na utaratibu mzuri juu ya matumizi ya fedha, mgawanyo mzuri wa majukumu, na sera nzuri za fedha zitakazo linda fedha ya biashara/taasisi na mali za biashara/taasisi dhidi ya ubadhilifu.

Katika uendeshaji biashara marazote utakutana na gharama za moja kwa moja na zili zisizo za moja kwa moja. Pia utakutana na gharama zinazotegemea na kuendana na kiwango cha uzalishaji ulichonacho, lakini pia kuna zile ambazo haitegemei uzalishaji upoje hizi ni gharama za kudumu mfano kodi ya pango.

Katika Makala hii tutaangazia kwa kifupi juu ya namna ya kuthibiti gharama za uendeshaji biashara yako kutegemea aina ya gharama na vyanzo vyake.
Faida za uthibiti gharama za uendeshaji biashara
• Kuboresha na kuongeza kiasi cha faida katika biashara yako
• Kunaongeza ufanisi wa uendeshaji biashara yako
• Kuna refusha na kuongeza uhai wa biashara yako
• Ni njia mbadala wakati wa hali mbaya ya kiuchumi inayoathiri biashara yako.
Zifuatazo ni hatua katika kuthibiti gharama za uendeshaji Taasisi/biashara yako

Hatua #1: AINISHA GHARAMA ZA BIASHARA YAKO

Jambo la kwanza ni kuhakikisha una tambua gharama zote zinazohusu biashara yako na kuziainisha moja baada ya nyingine, kuingana na ukubwa wa gharama hizo.
Hatua#2: ZITAMBUE ASILI/TABIA YA GHARAMA ULIZO NAZO

Hatua hii inalenga kutaka kujua ni nini visababishi vya gharama ulizo nazo. Katika hatua hii jiulize maswali yafuatayo.

·          Je gharama hii inategemea nini ?

·          Nini kinasababisha kuongezeka ama kupungua kwa gharama hii ?

Hatua #3 : TATHIMINI UMUHIMU WA KUWEPO KWA GHARAMA HIYO
Hii ni hatua muhimu kwani itakusaidia kufanya maamuzi endapo unaweza kuiondoa gharama hiyo isiwepo ama la. Katika hatua hii jiulize maswali yafuatayo.

·          Je ni athari zipi zitakazo ikumba biashara yangu endapo hakutakua na hii gharama

·          Je kuna uwezekano wa kupunguza gharama hii

·          Je biashara nyingine kama yangu zina gharamia kiasi gani katika aina sawa na hii ya gharama ?

Baaada ya kufanya tathimini hiyo unaweza kujua kwa wepesi endapo unaweza kuiondoa hiyo gharama na kuokoa pesa ambazo zingeendelea kutumika pasipo ulazima wowote. Nakujikuta biashara/Taasisi yako ikiendelea kushamiri katikati ya hali tete ya kiuchumi.

Hivyo ni muhimu kufanya tathimini ya kina juu ya gharama za biashara ulizonazo katika biashara ama/taasisi yako kabla ya kukimbilia kufunga ama kuuza biashara yako. Jitahiti kuonana na wataalamu wanaoweza kufanya tathmini hiyo na kukupa majibu muafaka
.


 Kwa ufafanuzi na maelezo Zaidi wasiliana na mwandishi kwa anwani ifuatayo: 
Name:Johnbosco Mvile
Email: mvilej@gmail.com
Mobile phone: 0763895490